Saturday, June 25, 2011

Katiba mpya kuzinduliwa April 2014

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
KATIBA MPYA ambayo mchakato wake umeanza inatarajiwa iwe imekamilika na
kuzinduliwa rasmi Aprili 26, 2014 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya
Muungano, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema mjini Dodoma leo *(Jumamosi Juni
25, 2011)*.
Akifungua Semina Elekezi kwa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kuhusu mchakato wa
Katiba Mpya, kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, alisema hayo ndiyo
matarajio ya Serikali .
“Ni matarajio ya Serikali kuwa Katiba Mpya itakuwa imekamilika na
kuzinduliwa ifikapo tarehe 26 Aprili, 2014 katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.
Waziri Mkuu alisema kwamba kama mamboyote yatakwenda kama yalivyopangwa,
Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha
Bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa au
mwanzoni mwa Mkutano wa Tano Oktoba mwaka huu.
Aliwataka Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kutoa ushirikino wa kutosha kwa Tume
ya Kuratibu na Kusanya Maoni itakayoundwa ili kuwezesha mikutano ya hadhara
ya kukusanya maoni kufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kuhamasisha wananchi
kuhudhuria na kutoa maoni yao.
“Katika suala hili kubwa nala kitaifa, ni vyema viongozi wasiingize siasa na
wajiepushe kuwashawishi Wananchi katika kutoa maoni yao, bali wawaache watoe
maoni kwa uhuru au pasipo shinikizo lolote,” alisema.
Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika
hatua ya awali, Serikali imeandaa rasimu yaMuswada wa Sheria ya Mapitio ya
Marekebisho ya Katiba *(The ConstitutionalReview Act*) ya Mwaka 2011.
(zaidi)
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa hatua ya sasa siyo kutunga Katiba Mpya bali ni
kuunda Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuelekea kutungwa kwa
Katiba Mpya.
(mwisho)
*Imetolewa na:*
* Ofisi ya Waziri Mkuu,*
* S.L.P. 980,*
* DODOMA*
*Jumamosi Juni 25, 2011*